Bondia anayefuata nyayo za Mayweather ahifadhi taji lake
Bondia anayefuata nyayo za aliyekuwa
bingwa wa dunia katika uzani wa middleweight Floyd Mayweather, Gervonta
Davis ametetea taji lake la uzani wa Super Featherweight kwa
kumuangusha Muingereza Liam Walsh katika raundi ya tatu ya pigano hilo
lililoandaliwa katika ukumbi wa Copper Box Arena.
Baada ya raundi mbili za tahadhari Davis alimrushia makonde mazito mpinzani wake yaliomuangusha.Walsh mwenye umri wa miaka 31 aliinuka lakini konde jingine la mkono wa kushoto kutoka kwa Davis mwenye umri wa miaka 22 lilimlazimu refa Michael Alexander kuingilia kati na kusimamisha pigano hilo.
Davis ambaye anakuzwa na Floyd Mayweather sasa hajashindwa katika mechi 18.
Hivi majuzi alimshinda kwa njia ya knockout bingwa katika uzani huo Jose Pedraza.
that is good
ReplyDelete