YALIYO JILI RUFAA YA SIMBA DHIDI YA TFF

                 RUFAA YA SIMBA FIFA  DHIDI YA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU TANZANIA                       (TFF)
Ikumbukwe SIMBA ilikata rufaa dhidi ya maamuzi yaliyo tolewa na shirikisho la soka nchini TFF.
Rufaa hiyo ilikua inahusu juu ya point tatu ambazo alipewa dhidi ya kagera sugar na kamati ya masaa 72 baada ya Kagera kuchezesha mchezaji mwenye kadi.
Baada ya kamati ya masaa sabini na mbili kuamua simba ipewe point tatu, TFF iliingilia kati swala hilo na kuipokonya Simba point hizo kwa madai kuwa kamati ya masaa 72 haikua na uhalari wa kutoa maamuzi juu ya pingamizi hilo.

Simba akiridhishwa na maamuzi ya TFF na ikaamua ku kata rufaa kwenye shirikisho la mpira wamiguu duniani FIFA.
Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii Simba ilionyesha documents walizo zipeleka FIFA kusaidia rufaa hiyo lakini hadi sasa hakuna majibu yaliyotolewa na simba juu ya rufaa hiyo.

Chakushangaza Raisi wa TFF bwana Jamal Malinzi alituma ujumbe kupitia mtandao wa twitter na kusema kua Raisi wa mpira wa miguu duniani FIFA anaipongeza Yanga kwa kuchukua kombe la vodacom jambo ambolo liliwaumiza sana mashabiki wa Simba na kuwafurahisha mashabiki wa jangwani.
 Kama taarifa zilizo tolewa na Raisi wa TFF ni za kweli basi ni dhahiri kuwa Rufaa ya Simba haina mashiko tena juu ya ubingwa wa yanga.


No comments

Powered by Blogger.