Historia ya Cristiano Ronaldo

         HISTORIA YA MCHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU CRISTIANO RONALDO

Jina lake kamili  ni Cristiano Ronaldo Dos Santos Aveiro, Mzaliwa wa portugal katika mji wa Santo Antonio.
Jina la Ronaldo alipewa na baba yake baada ya baba yake kuwa ana mpenda raisi wa zamani wa marekani Ronald Reagan ambeye alikua mwigazaji kabla na baba yake alimpenda sana na kuamua kumpa mwanae jina hilo.
Ronaldo aliishi maisha magumu sana mbaka kufikia kuishi chumba kimoja na dada zake na kaka zake.
Histiria yake ya mpira ilianza mwaka 1997 alipokua na umri wa miaka 12 alipo enda kufanya majaribio na timu ya Sporting Cp na kusainiwa kwa pound 1500.
Alipo fika miaka 14 Ronaldo alijiona kuwa an uwezo wa kuchuza mpira wa kulipwa na akakubaliana na mama yake kuwa aache shule ili aweze kujiusisha na mpira tu.\
Alipata umaarufu katika shule yake na siku moja alimlushia mwalimu wake kiti na ikawa sababu ya yeye kufukuzwa shule.
Mwaka mmoja mbele Ronaldo alipata tatizo la moyo ambalo lilimfanya aachane na mpira kabisa baati nzuri alipelekwa hospitali na kufanjiwa operation ambayo ilifanikiwa na kumfanya aendelee na mpira.
Kwa sasa Ronaldo ni Baba wa mtoto mmoja aliyezaliwa 17 June 2010 Aliyepewa jina la cristiano.
                            KUANZA KUTAMBULIKA BALANI ULAYA

Mwaka 2003 Ronaldo aliaanza kuonekana kwenye vyombo vingi vya habari nchini uingereza baada ya kuhusishwa na uhamisho wa club kubwa duniani kama Arsenal na Manchester utd na hatimaye kujiunga na Manchester united mwaka 2003.
Katika club ya Manchester united Ronaldo alifanikiwa kucheza michezo 196 na kufunga mogori 84
pia kufanikiwa kuchukua makombe yote ya nchini uingereza na kombe la UEFA na kuchaguliwa mchezaji bora wa Dunia mwaka 2008.
Mwaka 2009 ronaldo alijuanga na Real Madrid kwa dau ambalo alivunja rekodi za uamisho duniani kwa kipindi hicho.
Katiaka club ya Real madrida ronaldo amekuwa mchezaji bora mda wote kwa kuvunja rekodi ya club hiyo kwenye ufungaji wa ligi na Uefa champions league.
Hadi sasa ronaldo amechukua kiatu cha ufungaji bora barani ulaya mali nne pamoja na kuchukua tuzo ya mchezaji bora mara nne.
                           REKODI ANAZPO SIKILIA KWA SASA
Ronaldo ndiye mchezaji anaye ongoza kwa kufunga magoli mengi katika ligi ya UEFA champion league.
Ronaldo ana shikilia rekodi ya kua na magoli mengi katika club ya Real Madrid.
Ndiye mchezaji anaye ongoza kwa kuchukua kiati cha ufungaji bora mara nyingi zaida amechukua mara nne hadi sasa.
                                                 MWISHO
Bila kumlinganisha na mchezaji yoyote yule duniani kwa sasa Ronaldo ni moja ya mchezaji bora kabisa duniani katiak historia ya mpira.





2 comments:

  1. Kuna kijana wangu yupo vizuri sana naomba kupata ufadhiri wa shule kwani no kwanza anaumri wa miaka 2 lakini nihatari sana

    ReplyDelete

Powered by Blogger.